Baada ya Marc Cucurella kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 22 kwa kosa la kumvuta Harry Wilson wa Fulham aliyekuwa anashambulia lango la Chelsea huku Marc akiwa ndiye mtu wa mwisho wa timu (Chelsea) inayolinda, Chelsea imefikisha idadi ya Kadi nyekundu saba (7) kwenye mashindano yote msimu huu.
Kadi nyekundu ya Marc Cucurella imekuwa ya tano (5) katika Ligi kuu Engalnd msimu huu, wengine ni Moisés Caicedo (PL), Malo Gusto (PL), Trevoh Chalobah (PL), Robert Sánchez (PL) huku kadi nyingine ni Liam Delap (EFL) pamoja na Joao Pedro (UEFACL).
Kikosi cha Chelsea katika mchezo huo kilipoteza kwa idadi ya magoli 2-1 dhidi ya Fulham katika Uwanja wa Craven Cottage, ikiwa ni mchezo wa kwanza tangu wamfute kazi Kocha Enzo Maresca.
Chanzo; Eatv