Kamati ya Utendaji ya Yanga leo imekutana makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kujadili mradi wa ujenzi wa Uwanja.
Kikao hicho kimefanyika siku moja tu baada ya uongozi huo kukabidhiwa Hati ya kiwanja chao wanachotaka kuwekeza mradi huo kilichopo eneo la Jangwani, jirani na makao makuu ya klabu.
Makamu wa Rais wa klabu, Arafat Haji na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Gulamali hawakuhudhuria kikao hicho, lakini wakishiriki kwa njia ya mtandao.
Ikumbukwe jana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius John Ndejembi alikabidhi Hati ya kiwanja cha klabu hiyo wakati wa tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Mwanaspoti