Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mayweather, Pacquiao Kutwangana Tena Ulingoni

Mabondia maarufu duniani Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wamekubaliana kurudi ulingoni kuzichapa tena katika pambano la kitaalamu linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba, mwaka huu.

Pacquiao mwenye umri wa miaka (47), na Mayweather, (48), watapigana huko Las Vegas Jumamosi, ya Septemba 19, huku pambano hilo likionyeshwa moja kwa moja kwenye Netflix.

Itakuwa pambano la kwanza la kitaalamu kwa Mmarekani huyo tangu amshinde Conor McGregor raundi ya 10 ya pigano kwa ‘knockout’ tangu mwaka 2017.

Pacquiao wa Ufilipino alistaafu kutoka kwenye mchezo huo ili kujikita zaidi kwenye taaluma yake ya kisiasa mwaka 2021 lakini alirudi ulingoni Julai iliyopita kupambana na bingwa wa WBC wa uzito wa welterweight Mario Barrios, ambaye alihifadhi taji lake baada ya kutoka sare.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: