Lewis Hamilton ameshindwa kuhudhuria vipimo kwa ajili ya mashindano ya mbio za magari ya F1 ambayo yanafanyika nchini Italia baada ya mbwa wake anayejulikana kama Roscoe kuugua maradhi ya moyo.
Bingwa huyo wa mara saba wa dunia mwenye miaka 40, alikuwa amepangwa kukamilisha vipimo hapo jana lakini alishindwa kufuatia mkasa huo wa mbwa wake kuumwa. Sasa nafasi yake imechukuliwa na dereva mwenzake wa Ferrari, Zhou Guanyu.
Katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram, Hamilton aliwaomba wafuatiliaji wake wamuweke kwenye maombi mbwa wake huyo mwenye miaka
12.
Hata hivyo, Hamilton, ambaye alimaliza katika nafasi ya nane nchini Azerbaijan Jumapili iliyopita, anatarajiwa kurudi tena kazini wikiendi ijayo katika mashindano ya Singapore Grand Prix.
Chanzo: Dw