Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya Nyumba jijini Dodoma kwa mwanariadha wa kimataifa na Bingwa wa Dunia kwa Wanaume Sajinitaji Alphonce Simbu.
Hayo yamelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika hafla ya kumpongeza mwanariadha huuo iliyofanyika Septamba 27, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kushinda Mbio za Tokyo za KM 42 zilizofanyika nchini Japan na kutwaa medali ya dhahabu.
Mbali za zawadi ya nyumba Waziri Mkuu amemkabidhi Simbu hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 ikiwa ni zawadi kutoka kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kibo uliopo Hoteli ya Hyatt Regency jIjini Dar Es Salaam.
Chanzo: Eatv