Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy amejia juu kitendo cha Cristiano Ronaldo kwa kugomea mechi ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia kati ya Al-Nassr dhidi ya Al Riyadh akidai ni kitendo cha kibinafsi.
Taarifa zinaeleza kuwa Ronaldo alikuwa hakuridhishwa na mtazamo wa PIF na utaratibu wa kugawanya fedha, hasa kwa Al Hilal kupewa kiasi kikubwa kabla ya Kombe la Dunia la Klabu, huku Al-Nassr ikipata kidogo.
“Labda Ronaldo angeweza kutoa sehemu ya mshahara wake kwa klabu ili waweze kumiliki wachezaji zaidi. Sijawahi kusikia kitu cha kipuuzi kama hiki maishani mwangu, ni ubinafsi wa kupindukia.” - Murphy
Chanzo; Eatv