Timu za taifa za Uganda na Tanzania zimegawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Kundi C, katika michuano ya AFCON 2025.
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti huku Uche Ikpeazu akiisawazishia Uganda.
Bao la Msuva limempa rekodi tatu tamu kwa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Msuva kwanza amefikia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa Stars ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Mrisho Ngassa kwa muda mrefu.
Pili, Msuva ameendeleza pia rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyeifungia Taifa Stars bao katika awamu nyingi tofauti za AFCON ambapo hii ni mara ya tatu.
Rekodi ya tatu ambayo Msuva ameiweka ni ya kuwa mchezaji aliyefunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika kikosi cha Taifa Stars kwenye Fainali za AFCON.
FT: Uganda 🇺🇬 1️⃣🆚1️⃣ Tanzania 🇹🇿
Chanzo; Mwananchi