Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Alaba na Madrid Jua Kuzama Muda Wowote

Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kuachana na beki wake wa kimataifa wa Austria, David Alaba baada ya taarifa kubainisha kuwa mkataba wake hautaongezwa mara tu utakapomalizika.

uongozi wa Madrid umefikia uamuzi wa kutompa Alaba mkataba mpya hatua inayofungua ukurasa mpya katika safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Hispania.

Alaba alijiunga na Real Madrid mwaka 2021 akitokea Bayern Munich na amekuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho akichangia mafanikio kadhaa ikiwemo mataji ya ndani na kimataifa.

Changamoto za majeraha katika misimu ya hivi karibuni zimeathiri mwendelezo wake ndani ya kikosi.

Wakati huo huo, mustakabali wa mabeki wenzake wawili, Dani Carvajal na Antonio Rüdiger bado haujaamuliwa. Hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu iwapo mikataba yao itaongezwa.

 

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: