Klabu ya Simba Sc imethibitisha kuwa golikipa Moussa Pinpin Camara ambaye kwa sasa yupo Nchini Morocco kwa matibabu ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa Wiki 10 huku beki Abdulrazack Hamza ambaye na yeye anasafiri kwenda Morocco anaendelea na matibabu.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya Petro Atletico ya Angola utakaopigwa Jumapili Novemba 23, 2025.
“Mchezo wa Jumapili tutamkosa Moussa Camara ambaye yupo nchini Morocco alipokwenda kufanyiwa matibabu lakini pia tutamkosa beki wetu Abdulrazack Hamza ambaye na yeye anasafiri kwenda Morocco kwa matibabu zaidi. Taarifa njema ni kuwa Mohamed Bajaber amepona na hata mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania alianza na kucheza dakika 30".
Chanzo; Global Publishers