Kocha wa masumbwi Malik Scott, ameweka wazi namna anavyoweza kumsaidia mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, kuboresha hali yake ya kiakili katika hatua hii ya mwisho ya soka lake.
Scott ambaye alifunga ndoa na mtangazaji maarufu wa CBS Sports Kate Abdo mnamo Septemba 2024, ameweka wazi mpango huo, akimaanisha hitaji la kumsaidia Ronaldo ambaye bado anapendwa na mashabiki wake ulimwenguni kote.
Akiwa katika mahojiano na Canada Casino, Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44, amesema angefurahia kufanya mazungumzo ya kina na Ronaldo kuhusu maisha ya ushindani wa kiwango cha juu.
Ameongeza kuwa anafahamu changamoto za kiakili zinazowakumba wanamichezo wa kiwango cha dunia, na anaamini anaweza kuongeza kitu kwenye uwezo wa kiakili wa Ronaldo.
Chanzo: Mwanaspoti