Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, wametangaza mfumo mpya wa kurahisisha na kuharakisha mchakato wa kupata viza kwa mashabiki wanaopanga kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani.
Mfumo huo utawezesha kupunguza muda wa kupata viza kwa mashabiki wanaopanga kuhudhuria fainali hizo zitakazounguruma nchini Mexico, Marekani na Canada kuanzia Juni 11, 2026.
Mfumo huo utahakikisha mashabiki wanaopanga kwenda kuangalia mechi za Kombe la Dunia nchini Marekani watapewa kipaumbele katika kupata viza za utalii. Mchakato wa maombi na uhakiki bado ni uleule, lakini watafuta viza watapata miadi ya haraka zaidi.
Hata hivyo, shabiki atakayekuwa na tiketi ya mechi, hakutampa uhakika wa kuingia Marekani, bali kunasaidia kupata miadi ya haraka ya viza.
Trump na Infantino wanapendekeza kwamba kila mtu anayepanga kutembelea Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026 anapaswa kuanza mchakato huo mapema, badala ya kusubiri dakika za mwisho.
Chanzo; Mwanaspoti