Taarifa iliyotolewa na Simba SC jioni hii imeeleza kuwa aliyekuwa Kocha wao Fadlu Davids alikuwa wa kwanza kuomba kuondoka Klabuni hapo na Klabu imepokea ombi lake
“Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Mkuu Fadlu Davids baada ya kuhudumu na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Makubaliano haya ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu.”
“Klabu ya Simba inamshukuru Kocha Fadlu kwa kuiongoza Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumalizia nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya NBC.”
“Uongozi wa klabu unamtakia kheri na baraka kocha Fadlu katika maisha yake ya soka nje Simba.”
Kocha Fadlu amekuwa wa kwanza kutoa taarifa ya kuondoka Simba SC , muda mfupi baadae Klabu ya Raja Casablanca imemtambulisha kama Kocha wao mpya na baadae Simba wametoa taarifa kuwa hawapo tena pamoja na Fadlu
Chanzo: Clouds Media