Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aubameyang Kutua Chelsea Ulikuwa Uamuzi wa Hovyo

Staika Pierre-Emerick Aubameyang amedai kipindi chake cha hovyo alichokuwa nacho ni wakati alipohamia Chelsea, na ni kosa kubwa alilowahi kufanya kwenye maisha yake.

Fowadi huyo wa zamani wa Arsenal alifanya uamuzi wa kushtua wakati alipotua Stamford Bridge mwaka 2022 wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya umiliki mpya.

Akifunga mabao 92 katika mechi 163 alizochezea Arsenal, mambo makubwa yaliyatajiwa kutokea wakati mkali huyo wa Gabon alipokwenda kujiunga na Chelsea, hasa baada ya kukabidhiwa jezi yenye Namba 9 mgongoni.

Lakini, Aubameyang alishindwa kufikia viwango vya juu vilivyotarajiwa akijiunga na timu hiyo baada ya kipindi kifupi cha kuitumikia Barcelona.

Aliishia kufunga mabao matatu tu katika msimu wake wa kwanza wa hovyo kabisa, ulioishia kwenye kupigwa bei kwenye klabu ya Marseille ikiwa hata mwaka hajamaliza Stamford Bridge.

Akizungumzia hilo, Aubameyang amesema: “Yalikuwa makosa makubwa sana kwenda kule. Yalikuwa makosa makubwa.”

Na alipoulizwa kwa nini aliamua kujiunga Chelsea, aliongeza: “Kwa wakati ule, nilikuwa na wakati mbaya Barcelona. Nilivamiwa nyumbani na Barca ilihitaji kuuza mchezaji mmoja, mimi au Memphis Depay. Na ofa pekee iliyokuwa mezani ni Chelsea.

“Hivyo nilisema, ‘Sawa, kwa ajili ya familia yangu, nitaondoka hata kama ni Chelsea.’ Nilidhani kwamba ingekuwa sawa, Olivier Giroud alitoka Arsenal kwenda Chelsea na hakukuwa na tatizo. Lakini, kwa upande wangu mambo yalikuwa tofauti.”

Aubameyang alipata mafanikio makubwa alipotua Marseille baada ya kuachana na Chelsea. Alifunga mabao 30 katika mechi 51 huko Ufaransa kabla ya kwenda Al-Qadsiah ya Saudi Arabia. Na sasa mkali huyo mwenye umri wa miaka 36, amefunga mabao 21 huko Mashariki ya Mbali kabla ya kurudi Marseille, ambako amefunga mara tano katika mechi 14 alizocheza msimu huu.

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: