Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba ameondolewa kwenye kikosi cha AS Monaco kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).
Uamuzi huo umechangiwa na matatizo ya majeraha yaliyomkumba mchezaji huyo tangu ajiunge na klabu hiyo hali iliyomfanya acheze dakika 30 pekee katika mashindano yote tangu kuwasili kwake.
Maafisa wa klabu wameeleza kuwa Pogba bado hayupo katika hali bora ya kimwili kushindana katika kiwango cha juu cha mashindano ya Ulaya na juhudi zikiendelea kuhakikisha anarejea kikosini akiwa fiti kikamilifu.
Chanzo; Bongo 5