Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mo Salah Apiga Pesa Bila Jasho

Mohamed Salah amefunga bao kubwa kwa kuingiza Pauni 45 milioni kutokana na mikataba ya udhamini na haki za matumizi ya picha zake.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool, ambaye wiki hii alipewa ofa ya mkataba wa mamilioni ya pesa kujiunga na Ligi Kuu Saudi Arabia, alipata Pauni 8 milioni msimu uliopita pekee. Adidas, Pepsi, Vodafone, Uber na Oppo ni kati ya kampuni ambazo ana mikataba yenye faida kubwa.

Nyaraka za hivi karibuni za kampuni ya Salah UK Commercial zinaonyesha kuwa nyota huyo ana mali zenye thamani ya Pauni 44,557,359 katika kampuni hiyo.

Hiyo ni zaidi ya Pauni 150,000 kwa wiki kutokana na mapato ya nje ya uwanjani, mbali na mshahara wake wa Pauni 400,000 kwa wiki.

Pia inaonyesha ongezeko la Pauni 5 milioni ikilinganishwa na msimu uliotangulia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kutoka Misri pia aliongeza mapato yake kwa kuingiza mamilioni ya pauni kama bonasi baada ya kuiongoza Liverpool kushinda taji la Ligi Kuu England msimu uliopita. Nyaraka za karibuni za Salah UK Commercial zinaonyesha kuwa alilipa Pauni 1.5 milioni kama kodi na VAT.

Salah alifungua kampuni yake mwaka 2014 alipokuwa akichezea Chelsea na sasa ana mikataba yenye faida kubwa na Adidas, Pepsi, Vodafone, Uber na Oppo. Mapato yake yanaweza kuongezeka zaidi ikiwa atakubali dili la kujiunga na klabu ya Saudia, Al-Ittihad.

Alikataa uhamisho baada ya klabu hiyo kutoa ofa ya Pauni 150 milioni miaka mitatu iliyopita, lakini kulingana na ripoti, sasa amempa wakala wake ruhusa ya kuanza mazungumzo ya mkataba. Salah pia alihusishwa na uwezekano wa kuondoka Anfield msimu uliopita kabla ya kusaini nyongeza ya mkataba wa miaka miwili yenye thamani ya Pauni 42 milioni.

Hii ina maana kuwa Al-Ittihad italazimika kulipa fedha hizo kwa ajili ya nyota huyo bila kujali msimamo wake kuhusu uhamisho. Mustakabali wa Salah ulikuwa mada ya mjadala mwezi Desemba baada ya kutokea mzozo kati yake na kocha wa Liverpool, Arne Slot. Wakayamaliza.

 

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: