Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Messi Ajutia Kutojifunza Kiingereza Utotoni

Lionel Messi amekiri kuwa anajutia kutokujifunza Kiingereza alipokuwa mdogo.

Messi 🗣
“Najutia mambo mengi, Kutokujifunza Kiingereza nikiwa mtoto ni mojawapo."

"Nilikuwa na muda wa kusoma hata kwa kiwango cha msingi lakini sikufanya hivyo,ajutia sana.”

Messi alieleza kuwa katika maisha yake amewahi kukutana na watu mashuhuri na wenye mafanikio makubwa lakini wakati mwingine alijikuta akishindwa kuzungumza nao kwa uhuru kwa sababu ya lugha na jambo hilo limemfundisha somo kubwa kama mzazi.

“Ukiwa mdogo hutambui umuhimu wake, Leo ninachowaambia watoto wangu ni kusoma kuwa na elimu nzuri na kujiandaa kwa maisha.”

Lionel Messi amesisitiza kuwa watoto wake wana nafasi tofauti na aliyokuwa nayo alipokuwa akikua hivyo wanapaswa kutumia fursa hizo kikamilifu.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: