Pongezi za dhati kwa Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa kwanza, kwa mara ya pili mfululizo, na Emmanuel Dinday kwa kuwa mshindi wa tatu katika Mbio Ndefu za Daegu (Daegu Marathon) 2026 zilizofanyika nchini Korea Kusini.
Mlijiandaa vizuri, mmejituma kwa bidii na mmestahili ushindi. Mafanikio haya yanaimarisha hadhi yenu ya kimichezo kimataifa, yanaitangaza na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania, na pia ni funzo na hamasa kwa wanamichezo wengine na timu zetu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Serikali itaendelea kuweka na kuimarisha mazingira yatakayowawezesha kufanya maandalizi mazuri na kuwa washindani bora kote mnakokwenda.
Chanzo; Tanzania Journal