Mashabiki wa soka barani Ulaya wameanza kurejea kumbukumbu za fainali ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 baada ya droo ya hatua ya 16 bora ya ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuzikutanisha tena Chelsea na PSG.
Droo hiyo iliyopangwa na UEFA imeibua mjadala mkubwa, hasa ikizingatiwa historia ya karibuni kati ya miamba hiyo miwili ya Ulaya.
Katika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 iliyochezwa nchini Marekani, Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG), matokeo yaliyowashangaza wengi na kuwapa ubingwa huo wa dunia wa ngazi ya klabu.
Sasa, miamba hiyo inakutana tena katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi zitakazochezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.
Kupangwa kwa pambano hilo kumezua maswali mengi miongoni mwa wachambuzi na mashabiki.
je, PSG itafanikiwa kulipa kisasi cha kipigo kizito cha mabao matatu, au Chelsea itaendeleza ubabe wao dhidi ya mabingwa hao watetezi?
Hakuna shaka kuwa mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, presha ya kisasi, na mvuto wa kipekee, huku kila timu ikisaka tiketi ya kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu barani Ulaya.
Chanzo; Mwanaspoti