Kocha maarufu wa kimataifa José Mourinho ameripotiwa kuwa katika orodha ya makocha wanaotarajiwa kupewa jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Ureno mara baada ya kumalizika kwa mkataba wa kocha wa sasa Roberto Martínez kufuatia Kombe la Dunia la FIFA lijalo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na ESPN, viongozi wa Shirikisho la Soka la Ureno (FPF) wanatajwa kuvutiwa na uwezekano wa kumkabidhi Mourinho jukumu hilo endapo Martínez hataendelea na kazi yake baada ya mashindano hayo makubwa ya dunia.
José Mourinho kwa sasa anaendelea na majukumu ya klabu barani Ulaya ni mmoja wa makocha wenye wasifu mkubwa zaidi duniani na amewahi kushinda mataji makubwa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu England, Serie A na La Liga.
Licha ya mafanikio hayo Mourinho hajawahi kuinoa timu ya taifa katika taaluma yake ya ukocha.
Ripoti hizo zimeibua mjadala mpana miongoni mwa wadau wa soka nchini Ureno ambapo baadhi wanaona uteuzi wa Mourinho ungekuwa hatua sahihi kutokana na uzoefu na haiba yake ya kiuongozi, huku wengine wakieleza wasiwasi kuhusu falsafa yake ya uchezaji katika ngazi ya timu ya taifa.
Chanzo; Bongo 5