Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uongozi Simba Wakutana na Wachezaji, Benchi la Ufundi

Uongozi wa klabu ya Simba leo umekutana na wachezaji na benchi la Ufundi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumanne kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Ally Mangungu kwa pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Wakurugenzi, Crestentius John Magori.

Kikao hicho kinafanyika siku tatu baada ya tamasha la Simba Day, klabu ikitambulisha kikosi chake kamili cha msimu mpya na kucheza mechi ya kirafiki dhidi y Gor Mahia ya Kenya ambayo walishinda 2-0.

Taarifa ya Simba juu ya kikao hicho imesema ni kupanga mikakati ya msimu ambao watauanza Jumanne kwa mchezo dhidi ya Yanga.

 

Chanzo: Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: