Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mzize Apelekwa Afrika Kusini, Majeraha Yamtesa

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, yuko Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia kuumia tena akiwa mazoezini.

Mzize ambaye yuko nje ya uwanja kwa muda mrefu, aliumia tena muda mchache kabla timu yake haijasafiri kuelekea Lindi kuifuata Namungo mapema wiki hii.

Taarifa kutoka Yanga zimesema upo uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo akafanyiwa upasuaji mwingine ili kutibu haraka jeraha linalomkabili.

“Tunavyozungumza tayari Mzize yuko Afrika Kusini, uamuzi wa kwenda huko umelenga kuharakisha matibabu yake, lakini pia kumweka katika nafasi nzuri ya kurejea uwanjani mapema,” kimesema chanzo chetu.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: