Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Pantev Atajwa Kutua Simba, Aaga Gaborone

Gaborone United imetangaza kuachana rasmi na Kocha wake Mkuu, Dimitar Pantev ambaye inaripotiwa yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Simba.

Taarifa iliyotolewa na Gaborone United leo asubuhi, imeeleza kwamba Pantev ameomba kuvunja mkataba kwa ombi la haraka na wamelazimika kukubaliana na ombi lake.

"Klabu ya Mpira wa Miguu ya Gaborone United inapenda kutangaza rasmi kwamba Kocha Mkuu Dimitar Pantev ataachana na klabu ndani ya muda mfupi.

"Kocha Pantev ameitaarifu klabu juu ya nia yake ya kupata fursa mpya katika taaluma ya ukocha na baada ya kujadiliana na uongozi, Gaborone United kwa heshima imebariki ombi lake.

Asubuhi hii, Kocha Pantev amewaaga wachezaji na maofisa wa timu katika viwanja vya mazoezi vya klabu," imefafanua taarifa hiyo ya Gaborone United.

Gaborone United imemuelezea Kocha Pantev kama mtu aliyeiletea maendeleo makubwa klabu hiyo na kuifanya iwe bora.

"Tangu alipojiunga na klabu, Kocha Dimitar Pantev amekuwa nguzo ya uongozi wa kiweledi na mafanikio. Chini ya uongozi wake, Gaborone United ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu katika msimu wa 2024/2025 ukiwa ni wa nane katika historia, mafanikio makubwa ambayo yameimarisha jina lake katika historia ya kifahari ya klabu.

"Kwa niaba ya wakurugenzi wa klabu, timu ya ufundi, wachezaji, maofisa na familia nzima ya Gaborone United, tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Kocha Pantev kwa mchango wake mkubwa na kujitolea kusiko na kifani.

Heshima yake itabakia katika stori ya kifahari ya klabu yetu.

"Tunamtakia kila la kheri katika ukurasa wake mpya na mafanikio endelevu katika safari yake ya ukocha," imefafanua taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika ndani ya Simba, Pantev ndiye atakuwa Kocha Mkuu kwa ajili ya kuziba pengo la Fadlu Davids ambaye hivi karibuni alijiunga na Raja Casablanca ya Morocco.

Inaripotiwa kwamba Simba imevutiwa naaina ya soka la kushambulia kwa kasi na pasi ambalo Pantev ameifanya Gaborone United ilicheze katika msimu uliopita na msimu huu.

 

Chanzo: Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: