Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Philippe Coutinho ambaye alikuwa nahodha wa klabu ya CR Vasco da Gama ameomba kuvunja mkataba wake na klabu hiyo akieleza kuwa anahitaji kuipa kipaumbele afya yake ya akili.
Philippe Coutinho
“Nilihisi na kutambua kwamba maisha yangu katika klab yamefikia mwisho na niliamua kutorejea ili kuweka mbele afya yangu ya akili na ukweli ni kwamba nimechoka sana kiakili.
"Siku zote nimekuwa mtu wa faragha hivyo kuzungumza waziwazi hapa si rahisi lakini nahitaji kuwa mkweli."
"Nitabeba Vasco milele moyoni mwangu katika historia yangu na katika maisha yangu na kutoka moyoni, Asanteni kwa kila kitu.”
Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka wengi wakimpongeza kwa ujasiri wa kuzungumzia kwa uwazi changamoto za afya ya akili jambo ambalo mara nyingi wanamichezo hulikwepa.
Chanzo; Bongo 5