Cristiano Ronaldo yuko kwenye hatari kubwa ya kupigwa marufuku kucheza angalau mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia 2026 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza katika historia ya uwepo wake kwenye timu ya taifa.
Kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za FIFA, wachezaji wanaokutwa na makosa ya serious foul play hukumbana na adhabu ya angalau mechi mbili.
Ikiwa tukio hilo litahesabika kama violent conduct, adhabu inaweza kuwa angalau mechi tatu, au zaidi endapo litatajwa kama kitendo cha kushambulia mwamuzi au mchezaji, ikiwemo kupiga kiwiko au shambulio lingine lolote la aina hiyo.
Chanzo; Global Publishers