Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amefichua kuwa aliwaambia wachezaji wake wasahau matokeo ya 2-2 ya Arsenal dhidi ya Sunderland, kabla ya mechi yao dhidi ya Liverpool jana Jumapili, Novemba 9, 2025.
Arsenal ililazimishwa sare ya 2-2 dhjidi ya Sunderland juzi Jumamosi, Novemba 8, 2025, matokeo ambayo yalitoa ahueni kwa Man City iliyokuwa bado haijacheza dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Etihad.
Matokeo hayo yalifungua nafasi kwa Manchester City au Liverpool kufuatilia nafasi ya juu katika jedwali la ligi.
Hata hivyo, Guardiola amefichua alichozungumza na wachezaji wake, baada ya mechi ya Liverpool ambayo ilikubali kichapo cha 3-0, na kuendelea kutoa mwanya kwa miamba hiyo ya Jiji la Manchester kuingia katika mbio za ubingwa sambamba na Arsenal.
Guardiola amesema alitambua wachezaji wake walifurahishwa na matokeo ya Arsenal, lakini alichokifanya ni kuwarudisha katika mawazo ya mechi iliyokuwa inawakabili, ambayo pia ilitakiwa washinde ili kuingia kwenye mbio za ubingwa msimu huu.
Chanzo; Mwanaspoti