Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wayne Rooney Amtabiria Mabaya Arteta

Gwiji wa Ligi Kuu England, Wayne Rooney, ameonya kuwa Mikel Arteta anaweza kufukuzwa kazi endapo atashindwa kuipa Arsenal taji la Ligi Kuu msimu huu

Arsenal kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi sita mbele ya Manchester City, na imekuwa vinara wa kubashiriwa kushinda taji lao la kwanza tangu mwaka 2004. Kwa mujibu wa Rooney, nafasi hiyo nzuri inaondoa kabisa visingizio kwa Arteta.

Akizungumza kwenye kipindi cha The Wayne Rooney Show, amesema: “Arsenal wamemuunga mkono Arteta kwa kiwango kikubwa na wamempa kikosi bora sana. Kama hawatashinda mwaka huu, kutakuwa na presha kubwa kwake, bila shaka.”

Rooney pia anaamini ushindi wa kusisimua wa Man City dhidi ya Liverpool Anfield unaweza kuwa umeathiri kisaikolojia kikosi cha Arteta. City ilirejea kutoka nyuma na kushinda 2-1, hali iliyopunguza pengo kutoka pointi tisa hadi sita.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: