Mwanasoka nguli Cristiano Ronaldo amehitimisha mgomo wake wa mechi kadhaa kwenye klabu yake ya Al Nassr ya kule Saudi Arabia. Aligomea mechi mbili mfululizo baada kutokuridhishwa na yanayoendelea klabuni kwake hasa kutokana na uhaba wa fedha ambao umeathiri hata usajili wa wachezaji wapya. Kingine kinachoelezwa kuwa kilimkasirisha sana Ronaldo ni hatua ya klabu ya Al Hilal ambayo ni hasimu mkubwa wa klabu yake kumsajili Karim Benzema, aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake Ronaldo wakati wakiwa Real Madrid.
Ronaldo aligomea pia kile kinachosemekana kuwa ukosefu wa usawa ndani ya klabu yake hasa kitendo cha wafanyakazi wengine wa klabu hiyo kucheleweshewa mishahara mara kadhaa.
Baada ya kukosa mechi mbili za ligi kwa mgomo, Cristiano Ronaldo sasa amerudi kwenye mazoezi na anatarajiwa kuiongoza Al Nassr Jumamosi dhidi ya Al Fateh.
Chanzo; Dw