Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa Amezitakia kheri klabu za Tanzania Simba, Yanga pamoja na Singida Black Stars ambazo hii leo zinashiriki katika mashindano ya kimataifa barani Afrika ngazi ya klabu bingwa na shirikisho.
Msigwa akiwasilisha Salamu za heri kwa niaba ya serikali amesema kuwa goli la mama liko pale pale na Rais Ameamua kuwa zawadi hiyo ya Goli la mama ianze kutolewa katika hatua za awali kabisa ambapo kila goli la ushindi ni shilingi milioni tano hivyo kila klabu itakayoshinda itapokea kadiri ya magoli itakayoshinda ambapo hatua ya robi fainali Goli la mama litakuwa milioni 10 na hatua ya nusu fainali goli la mama litakuwa milioni 20 na fainali itaandaliwa zawadi maalum huku ushindi wa matuta utahesabiwa kama goli moja.
“Ninatambuwa kuwa Yanga leo itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wiliete nchini Angola, mechi zinazofuata ni Simba watakaocheza dhidi ya Gaborone ya Botswana, Azam watakuwa nchini sudan wakicheza dhidi ya El-Merriekh na Singida black stars watakuwa nchini rwanda wakicheza na Rayon Sports tunawatakia kila la kheri na goli la mama liko pale pele tena kwanzia hatua hizi za awali” amesema Gerson Msigwa.
Chanzo; Millard Ayo