Tanzania imeajiandaa vilivyo kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa mshindano makuu ya mpira barani Afrika ya CHAN. Hayo yamesemwa na Katibu wa BMT, Neema Msitha wakati akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa Clouds TV.
"Maandalizi hayakuwa mepesi na tunafanya hizi kazi kwa kuangalia viwango ambavyo vimewekwa na wenye shindano lao. "Hili shindano la Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika kwa hiyo anapokupa uenyeji wa mashindano kunakuwa na conditions wanakupa. Kwamba kwenye eneo la miundombinu ya viwanja wanataka iweje.
"Kuanzia hotel, usafiri, watendakazi pia. Najisikia fahari kwa kusema kwa kiasi kikubwa mambo yote ambayo wametuelekeza kuyafanya, tumeyafanya na kuyakamilisha kwa level ambazo wanazitaka wao. "Na siku mbili zilizopita alikuja Katibu Mkuu wa CAF na yeye alipita na kusema Tanzania ipo tayari hata Jana tungeweza kupuliza filimbi”, amesema Msitha.
Tazama mahojiano haya kupitia YouTube ya Clouds Media.