Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uchaguzi Kuamua Hatma ya Lewandowski, Barcelona

Mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, 37, ameamua kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais wa Barcelona unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.

Lewandowski anahusishwa na ofa kadhaa zikiwemo AC Milan, Atletico Madrid, Chicago Fire, Fenerbahce, pamoja na Saudi Arabia.

Uongozi mpya wa Barcelona unaweza kuamua kumpa mkataba mpya kwa masharti mapya au kuidhinisha kuondoka kwake ili kupunguza mzigo wa mishahara.

Licha ya umri wake, Lewandowski bado anaamini ana uwezo wa kucheza soka la ushindani wa juu, hivyo kipaumbele chake cha kwanza kwa sasa ni kubaki Barca kabla ya kufikiria kuondoka.

Awali, iliripotiwa kwamba straika huyo angeachwa na Barca mwisho wa msimu huu kwa ajili ya kupunguza gharama za ulipaji mishahara na kupata nafasi ya kumsajili kwa mkataba wa moja kwa moja Marcus Rashford ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Nou Camp.

Mkataba wa Lewandowski unatarajiwa kumalizika ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: