Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Olunga Aingia Orodha ya Matajiri Afrika Mashariki

Mshambuliaji nyota wa Kenya, Michael Olunga, anaendelea kuthibitisha ubora wake ndani na nje ya uwanja baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa wachezaji matajiri zaidi Afrika Mashariki, kufuatia mafanikio yake makubwa akiwa na klabu ya Al Arabi SC nchini Qatar.

Kwa mujibu wa taarifa za michezo, Olunga analipwa takribani euro milioni 5.8 kwa mwaka sawa na zaidi ya shilingi bilioni 17 za Kitanzania hali inayomweka kwenye orodha ya wachezaji wa Afrika Mashariki wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.

Mafanikio yake yanafananishwa na yale ya nahodha wa zamani wa Kenya, Victor Wanyama, huku Olunga akitajwa kuwa fahari ya soka la Kenya na mfano wa kuigwa kwa vijana wengi wa ukanda huu.

 

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: