Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

CAF Yaanza Uchunguzi Matukio ya Vurugu Robo Fainali Afcon

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeonyesha kukerwa na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyoonyeshwa katika mechi mbili za robo fainali ya AFCON 2025 zilizochezwa Ijumaa na Jumamosi huko Morocco.

Mechi hizo ni Morocco dhidi ya Cameroon iliyochezwa Ijumaa, Januari 9, 2026 na nyingine baina ya Nigeria na Algeria iliyochezwa, Jumamosi, Januari 10, 2026.

Taarifa iliyotolewa na CAF leo, Jumatatu, Januari 12, 2025 imeeleza kuwa Shirikisho hilo limeanzisha uchunguzi kwa baadhi ya matukio ya utovu wa nidhamu yaliyohusisha, wachezaji, maofisa wa timu na waandishi wa habari kwenye mechi hizo.

“CAF imekusanya ripoti za hivi karibuni za mechi pamoja na ushahidi wa video unaoonyesha kuwepo kwa vitendo vinavyoweza kuwa visivyokubalika vilivyofanywa na baadhi ya wachezaji na maofisa, na imefungua uchunguzi kuhusu matukio yaliyotokea wakati wa mechi za robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

“CAF imepeleka masuala hayo kwa Bodi ya Nidhamu kwa ajili ya uchunguzi na imesisitiza kuchukuliwa kwa hatua stahiki endapo watu waliotajwa watabainika kuwa na hatia ya ukiukwaji wowote.

“CAF pia inapitia picha za video za tukio linalohusisha wanahabari ambao inadaiwa walifanya vitendo visivyofaa katika eneo la mchanganyiko,” imefafanua taarifa hiyo ya CAF.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: