Rais wa Club ya Yanga Injinia Hersi Said, ameteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano yote ya Vilabu vya Wanaume Duniani kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2025-2029 ambapo uteuzi huo unamfanya kuwa Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na kati kuingia kwenye kamati kubwa ya mpira Ulimwenguni.
Uteuzi huo umetokana na maamuzi ya Baraza la FIFA yaliyofanyika tarehe 2 Oktoba 2025, ambapo Eng. Hersi Said amepata nafasi hiyo kwa kutambua mchango na uwezo wake katika maendeleo ya soka na anatarajiwa kushiriki kikamilifu katika kupanga na kusimamia mashindano ya Klabu za Wanaume katika ngazi ya kimataifa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha na kuendeleza soka duniani.
Chanzo; Millard Ayo