Bondia Anthony Joshua anatarajiwa kustaafu mchezo wa masumbwi baada ya kunusurika katika ajali mbaya ya gari iliyosababisha vifo vya marafiki zake.
Mjomba wa Anthony Joshua anayefahamika kwa jina la Ademola Johua amedai kuwa bingwa wa zamani wa dunia amewaeleza familia yake kuwa atastaafu ndondi kufuatia ajali mbaya ya gari iliyowaua marafiki zake wawili wa karibu.
Adedamola Joshua
“Jambo kubwa zaidi ni kwamba atastaafu ndondi. Hilo ni jambo moja linalotufanya tufurahi kwa sababu kila anapopigana ulingoni, sisi huwa tunaguswa sana kihisia,” alisema mjomba wake,
“Kila anapoangushwa, ni kama moyo unatoka kifuani mwetu. Hisia zote hizo na maumivu kila anapopigana ni kiwewe kikubwa sana kwetu pia.
"Sasa kwa kuwa amesema atastaafu sisi kama ndugu zake hatuna budi zaidi ya kufurahi".
Chanzo; Bongo 5