Ndege ya Shirika la Tanzania ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo Januari 8, 2025 ikiwa na msafara wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ikirejea kutoka Morocco ilikoshiriki Fainali za Mataifa Afrika AFCON 2025.
Stars iliishia hatua ya 16-Bora baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco.
Timu hiyo imepokewa na Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi aliyefuatana na viongozi wengine wa Serikali.
Chanzo; Mwananchi