Shirikisho la Soka Ulimwengini (FIFA), limezindua rasmi picha maalum ya Kombe la Dunia 2026.
Picha hiyo mpya imevutia mashabiki kote duniani kwa kubeba picha za wachezaji mashuhuri kutoka pande zote za dunia, ikiwemo nyota wa Afrika.
Mashabiki wanashauriwa kuangalia kwa makini ili kutambua wachezaji kutoka bara la Afrika waliowekwa kwenye picha hiyo, hatua inayoongeza msisimko na kujenga uhusiano wa karibu kati ya mashindano hayo na wapenzi wa soka barani humo.
Hii ni fursa kwa wapenzi wa soka barani Afrika kusherehekea ushawishi wa nyota wa Afrika katika jukwaa la kimataifa na kuonesha umahiri wao kwenye mashindano makubwa zaidi ya soka duniani.
Chanzo; Mwanaspoti