Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, Eric Chelle, anatafakari orodha ya wachezaji atakaowaita kwa ajili ya mechi ya mchujo ya kufuzu kombe la dunia 2026 barani Afrika.
Nigeria inatarajia kucheza dhidi ya Gabon Novemba 13, 2025, kwenye Uwanja wa C.S. Prince Héritier Moulay El Hassan, uliopo Rabat, Morocco. Mshindi wa mchezo huo atachuana na mshindi wa mchezo kati ya Cameroon na DR Congo katika hatua inayofuata ya mchujo wa Afrika.
Ingawa Chelle amekuwa akikosolewa kwa uteuzi wa wachezaji na mbinu zake, kocha huyo raia wa Mali anaonekana kupata dawa ya tatizo hilo, kupitia mechi za hivi karibuni.
Chini ya uongozi wake, Super Eagles imepata ushindi mara nne na sare mbili katika mechi sita za mashindano, wakikusanya pointi 14 kati ya pointi 18 ambazo zingewavusha moja kwa moja hadi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.
Chanzo; Mwanaspoti