Tottenham bado inatamani sana kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, dirisha lijalo la majira ya baridi.
Inaelezwa Spurs ipo tayari kulipa zaidi ya Pauni 70 milioni kama ada ya uhamisho ya fundi huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.
Rodrygo amekuwa akihusishwa kuondoka Madrid tangu kuanza kwa msimu huu kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza cha timu hiyo na Kocha Xabi Alonso anaonekana hayupo katika mipango yake.
Licha ya mara kadhaa kocha huyo kusisitiza bado anahitaji huduma ya Rodrygo, mara nyingi staa huyo ameonekana kukalishwa benchi na kuingizwa katika dakika za mwisho kwa baadhi ya mechi.
Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza jumla ya mechi 16 za michuano yote na hajafunga bao hata moja zaidi ya asisti nne alizotoa.
Mbali ya Spurs, Rodrygo pia anawindwa na Inter Milan ya Italia lakini kiasi cha pesa kinachohitaji ili kumnunua kinaonekana kikwazo.
Chanzo; Mwanaspoti