Klabu ya Inter Miami imethibitisha kuwa nyota wao, Lionel Messi, atakosa mazoezi ya siku kadhaa za maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’ kufautia majeraha ya misuli (muscle strain) ya nyuma ya paja la mguu wa kushoto yanayomsumbua kwa sasa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo, Messi alifanyiwa vipimo vya ziada vilivyothibitisha tatizo hilo.
Kurejea mazoezini kwa mshambuliaji huyo raia wa Argentina kutategemea maendeleo yake kiafya na tathmini ya kitabibu katika siku zijazo.
Habari hiyo imeibua wasiwasi kwa mashabiki wa soka duniani, huku wengi wakimtumia salamu za kumtakia nafuu ya haraka nahodha huyo wa Argentina.
Tunamtakia Messi apone haraka na kurejea uwanjani akiwa imara zaidi.
Chanzo; Mwanaspoti