Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, ameripotiwa kuwa hana mpango wa kurejea Manchester United baada ya kumalizika kwa mkopo wake katika klabu ya FC Barcelona.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mirror, Rashford yuko tayari kupunguza mshahara wake ili aendelee kusalia Hispania, akiamini maisha na mazingira ya soka Barcelona yanamfaa zaidi kwa sasa.
Hatua hiyo inaashiria wazi kuwa nyota huyo hana tena nia ya kurudi Old Trafford, huku akitafuta ukurasa mpya wa maisha yake ya soka barani Ulaya.
Chanzo; Global Publishers