WINGA wa Real Madrid, Vinicius Jr, 25, amewaambia viongozi wa timu hiyo anataka kulipwa mshahara sawa na ule ambao mshambuliaji mwenzake wa timu hiyo, Kylian Mbappe analipwa na kama takwa hilo halitatimizwa atalazimisha kuondoka mwisho wa msimu huu.
Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa pili akiwa na Madrid analipwa takribani Euro 600,000 kwa wiki wakati Vinicius akilipwa Euro 400,000 kwa wiki.
Vinicius amekuwa akihusishwa sana kuondoka hivi karibuni kutokana na hali yake katika kikosi hicho tangu kuwasili kwa kocha mpya Xabi Alonso ambaye mara kadhaa amekuwa akimweka benchi pamoja na kumfanyia mabadiliko kabla ya mechi kumalizika.
Hivi karibuni pia alisikika akitamka hadharani ni bora aondoke kauli ambayo aliitoa baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mechi ya El Classico dhidi ya Barcelona.
Waarabu wa Saudi Arabia pamoja na PSG ni miongoni mwa timu zinazoitamani.
Chanzo; Mwanaspoti