Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TFF Yaufungulia Uwanja wa KMC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa KMC, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya Kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.

TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja, ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: