Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mbappe Aikaba PSG Adai Pauni 200 Milioni

SUPASTAA straika, Kylian Mbappe anahitaji alipwe zaidi ya Pauni 200 milioni kutoka Paris Saint-Germain huku sakata hilo likifikishwa mahakamani.

Mbappe aliondoka Parc des Princes kwenda kujiunga na Real Madrid wakati mkataba wake ulipofika ukomo Juni 2024. Jambo hilo liliifanya PSG kukosa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo, kitu kilichomfanya mmiliki Nasser Al-Khelaifi kuchukia.

Lakini, gazeti la Ufaransa la Le Parisien limeripoti kwamba Mbappe anataka alipwe Pauni 211 milioni kutokana na kutokubaliana mambo fulani katika mchakato huo wa uhamisho wake.

Mbappe anawashutumu waajiri wake wa zamani kushindwa kufanya mkataba wake maalumu kuwa wa kudumu, huku wakishindwa kumlipa karibu Pauni 50 milioni ya mishahara yake na bonasi.

Lakini, PSG imemjibu Mbappe juu ya matakwa yake ya kulipwa Pauni 158 milioni ikidai ilifanya hivyo baada ya mchezaji huyo kuahidi asingeondoka kama mchezaji huru kwenye timu.

PSG ilisema ilipokea ofa ya zaidi ya Pauni 260 milioni kutoka kwenye klabu moja ya Saudi Pro League miezi 12 kabla ya staa huyo wa zamani wa Monaco kuondoka bure na alikataa uhamisho huo wa kwenda Saudi Arabia.

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: