Klabu ya Singida Black Stars imewasimamisha kazi kwa miezi mitatu wachezaji wake wawili, Khalid Aucho na Amas Obasogie, kufuatia tuhuma za utovu wa nidhamu na upangaji wa matokeo.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa, Februari 27, 2026 na Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo imeeleza kuwa Aucho amepewa adhabu ya utovu wa nidhamu pamoja na utoro kazini.
Golkipa Obasogie amesimamishwa kwa kipindi hicho hicho kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika na upangaji wa matokeo.
“Uongozi kupitia Kamati ya Nidhamu umechukua hatua hizi kwa mujibu wa kanuni na taratibu za klabu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Chanzo; Mwananchi