Nyota wa soka duniani Cristiano Ronaldo ametangaza rasmi kuanza safari mpya nje ya uwanja baada ya kuwa mmiliki mwenza wa klabu ya UD Almeria kwa kununua asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo ya Hispania.
Ronaldo 🗣
“Imekuwa ndoto yangu kwa muda mrefu kuchangia soka zaidi ya uwanjani na nina furaha kuwa mmiliki mwenza wa Almeria.”
"Almeria ni klabu yenye misingi imara na uwezo mkubwa wa kukua zaidi katika soka la Hispania na ninasisitiza kuwa nipo tayari kushirikiana na uongozi wa klabu hiyo katika hatua mpya ya maendeleo."
Hatua hiyo inaashiria mwanzo wa enzi mpya kwa mshambuliaji huyo wa Ureno ambaye kwa sasa anaendelea na maisha yake ya soka huku akipanua uwekezaji wake katika sekta ya michezo na biashara.
Chanzo; Bongo 5