Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Refa wa Taifa Stars Vs Morocco Aondolewa Afcon

Mwamuzi wa Kimataifa wa Mali, Boubou Traoré, ameripotiwa kuondolewa katika orodha ya waamuzi watakaosimamia mechi zilizosalia za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazoendelea Morocco.

Mbali na Traoré, mwamuzi mwingine aliyeripotiwa kuondolewa ni Abdou Abdel Medire kutoka Cameroon, ambaye pia hatasalia katika ratiba ya usimamizi wa michezo ya hatua zilizobaki za mashindano hayo.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni sehemu ya mchakato unaoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kufanya tathmini ya viwango na utendaji wa waamuzi waliokuwa wakisimamia michezo ya AFCON, ili kuhakikisha haki na ubora wa maamuzi katika hatua nyeti za mashindano.

Traoré anakumbukwa zaidi kwa kusimamia mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Taifa Stars na Morocco, mchezo uliogubikwa na maamuzi yaliyotajwa kuwa ya utata na kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika.

Miongoni mwa matukio hayo ni lile la kushindwa kuipa Taifa Stars mkwaju wa penalti katika dakika za lala salama, baada ya Adam Masina wa Morocco kumsukuma Iddi Selemani ‘Nado’ katika eneo la hatari.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: