Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefuzu hatua ya mtoano baada ya kutoa sare dhidi ya Tunisia katika mechi za AFCON 2025.
Stars imefuzu hatua hiyo baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye timu za 'best looser' juu ya Angola ambayo wamelingana pointi ikiwazidi mabao ya kufunga. Stars ina mabao 3 ya kufunga na 4 ya kufungwa huku Angola akiwa nayo 2 ya kufunga na 3 ya kufungwa.
Matokeo mengine, Uganda imeaga mashindano hayo ikikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Nigeria.
Chanzo; Mwanaspoti