Ikiwa imesalia takribani miezi 11 kuelekea kuanza kwa michuano ya kombe la Dunia 2026 ambayo itafanyika Marekani, Mexico na Canada, Rais wa Marekani Donald Trump amesema atahamisha mechi za Kombe la Dunia la 2026 kutoka miji ambayo si salama na kuipeleka katika miji salama.
Marekani itakuwa mwenyeji wa mechi 78 kati ya 104, ikiwa ni pamoja na fainali huku miji 11 ya ya taifa hilo imeratibiwa kuandaa mechi katika mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yatahusisha mataifa 48
Ikumbukwe Shirikisho la Soka Duniani FIFA ndilo lenye jukumu la kuandaa michuano hiyo na kuchagua miji itakayoandaa michuano hiyo na haijulikani kama Trump ana mamlaka ya kufanya mabadiliko hayo, licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na rais wa FIFA Gianni Infantino.
Miji 11 ya Marekani ambayo itandaa michuano hiyo ni Atlanta, Boston, Dallas, Houston, Kansas City, Los Angeles, Miami, New York/New Jersey, Philadelphia, San Francisco na Seattle.
Chanzo: East Afrika Radio