Klabu ya Kakamega Homeboyz FC ipo katika majonzi kufuatia kifo cha beki wao, Silas Abungana, aliyefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega.
Abungana alicheza na kumaliza dakika zote 90 katika mchezo wa ligi dhidi ya Mara Sugar FC uliofanyika siku ya Jumamosi jambo lililoongeza mshtuko mkubwa kwa mashabiki wachezaji na wadau wa soka.
Chanzo; Bongo 5