Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Afcon 2027 Kombe Kubaki Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Paul Makonda ameondoka nchini leo kuelekea Morocco ambako anakwenda kuupokea uenyeji wa AFCON 2027 ambapo amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amempa ujumbe wa kuupeleka kwa Rais wa CAF lakini pia ameagiza yeye na Timu yake wakajifunze mbinu kwa Morocco zitakazoifanya Taifa Stars ibebe kombe la AFCON 2027.

Akiongea na Waandishi wa Habari Airport Dar es alaaam leo January 16,2026, Makonda amesema “Leo nimepata heshima ya kutumwa na Rais Samia kwenda kupokea kijiti cha AFCON 2027, Rais Samia ametupata barua/ ujumbe mahususi wa kumpelekea Rais wa CAF kutokana na kazi nzuri ambayo CAF ilimpa tuzo kama Rais bora aliyefanya kazi nzuri na kuinua sports nchini”

“Kazi ya pili ambayo Rais ametutuma, amesema katazameni mbinu za Morocco kuhakikisha Tanzania 2027 kama sio Stars kucheza fainali basi kombe libaki Tanzania”

“Jambo la tatu Morocco ni nchi inaongoza kwa Utalii (Watalii wengi zaidi ya mil 15) kupitia michezo, Rais Samia anataka kupitia michezo Tanzania ishike namba moja kwa utalii, tatakuwa na wanaoangalia standard za hoteli, huduma za usafiri, vyakula n.k, kuhakikisha AFCON 2027 inaacha historia njema ya Watanzania kwa kuimarisha uchumi wao”

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: